Tuesday, March 20, 2012

Kwa wale ndugu zangu wenye tatizo la nguvu za kiume poleni kwa
maswahibu mnayo yapata lakini hampaswi kuvunjika moyo maana ufumbuzi
wa matatizo yenu uko mikononi mwenu.

Heshima ya mwanaume haiji kwa kula ugali mkubwa au kubeba vyuma vizito vya kutanulia misuli. Heshima ya mwanaume hujengwa juu ya mgongwa wa mwanamke, ndio maana katika mambo au jambo linaloweza kumkosesha raha mwanaume ni kujijua kuwa hawezi kumridhisha mwanaume kwa mapenzi.

kwa wale wenye matatizo ya kukosa urijali kwenye mahusiano yao hasa wanaume, hapa kuna tiba mbadala mnazo weza kuzitumia. Karibu ujisomee na kujiponya ili urudishe heshima nyumbani.

1. Kwa wale ndugu zangu mlioko maeneo ya pwani au pengine pweza
wanapopatikana kirahisi, jitahidini kupata supu ya pweza mara 3 au
hata 4 kwa wiki. Hapa ni supu pamoja na nyama yake, huna haja ya
kupiga mabakuli mengi, bakuli moja moja tu linatosha kwa siku. Hii
inarejesha heshima kunako uwanja wa seremala. Uwanja ule! Sijui nani
aliubuni walaah.

2. Dawa nyingine ni Juice ya tende (kwa lugha ya kina kameruni mwaita
dates, mtu yule!?). Tende zinapatikana sana hata kwenye
ma-supermarket. Nunua paketi za tende kiasi unachotaka, toa kokwa
zilizoko kwenye tende, pata kiasi cha tende zisizokuwa na kokwa kama
nusu birauli, chukua maziwa fresh birauli moja au mbili changanya
pamoja wenye brenda. Saga vyote kwa pamoja hadi upate juice. Ikiwa
tayari kunywa birauli 1 hadi 2 fanya hivyo mara kadhaa kila
unapojisikia. Ni nzuri kwa muda wa jioni na asubuhi.

3. Mchicha na tangawizi
Chambua mchicha vichanga vi-2 au vi-3, pata na tangawizi fungu moja
isage kisha weka mchanganyo huo kwenye sufuria, weka maji kiasi cha
kutosha mchanganyo huo kisha chemsha hadi viive. Ikiwa tayari kunywa
supu na mchicha wake.

Nitaendelea tena kwa sasa kazi njema na yenye mafanikio wote.

No comments:

Post a Comment